Mkoa wa
Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na
shirika serikali ya Uswizi leo Jumanne Desemba 13,2016 umezindua Mpango
wa Mzabuni teule “Mfumo wa Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi”.
Mfumo wa
Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja
‘Prime Vendor’ ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wa sekta binafsi na
serikali ukiwa na lengo la kujazia upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na
vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela
aliyekuwa mgeni rasmi alisema lengo la mfumo huo ni kuziba pengo
linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika
vituo vya afya kutoka Bohari kuu ya dawa.
Alisema
kutokana na bohari ya dawa ya serikali kutokidhi mahitaji kila
halmashauri hununua dawa kutoka kwa wazabuni wanaowataka matokeo yake
bei ya dawa inakuwa kubwa,mlolongo mrefu wa manunuzi na kukosekana kwa
njia rahisi ya usimamizi wa mfumo wa ugavi na usambazaji.
"Mkoa wa
Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya( HPSS Project)
unaofadhiliwa na serikali ya Uswizi kupitia shirika lake la Maendeleo
(SDC) umeamua kutafuta njia ya kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu
wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kutoka bohari kuu ya dawa kwa kutumia
mfumo wa manunuzi ya nje ya bohari kuu unaohusisha mzabuni mmojatu kwa
mkoa mzima,ambaye sasa Bahari Pharmacy Limited",alieleza Msovela.
Naye
mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana
Mapunjo alisema mkoa wa Shinyanga ni wa pili baada ya Mkoa wa Dodoma
kuanza kutekeleza Mpango wa Mzabuni teule huku akisisitiza halmashauri
kusimamia matumizi bora ya dawa na wazee kuendelea kupewa kipaumbele.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Mradi wa Tuimarishe
Afya (HPSS),mkurugenzi wa MSD,Mfamasia mkuu wa serikali,mganga mkuu wa
mkoa wa Shinyanga,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu
wa halmashauri na wageni mbalimbali.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 40 kutoka kwenye uzinduzi huo….Tazama Hapa Chini
Kwa
kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga
Dr. Harun Kasale,katikati ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli
Kapologwe na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo
Jumanne Desemba 13,2016 wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule
“Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi ambapo alisema
mfumo huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa
dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga .Aliongeza kuwa
bohari ya dawa ina uwezo wa kuhudumia wateja kwa asilimia 57 pekee
katika mkoa wa Shinyanga.
Wa kwanza
kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais
TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi
ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo
Wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment