Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
Watu
zaidi ya 400 wakazi wa mji wa Kahama na viunga vyake wamejitokeza kupima
VVU wakati wa mashindano ya Mahusiano Cup ambayo huusisha michezo ya
mpira wa miguu na mpira wa pete.
Mashindano
hayo ambayo huandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya Acacia
kupitia Mgodi wa Buzwagi yalizinduliwa tarehe moja desemba, yakiwa na
lengo la kuhamasisha Jamii kupima afya zao na kuimarisha uhusiano baina
ya wenyeji na Mgodi wa Buzwagi.
Akizungumza
wakati wa Kuhitimisha fainali za michezo hiyo pamoja na kampeni ya
upimaji VVU katika uwanja wa mpira wa Kahama Mji, Katibu Tawala wa
Wilaya ya Kahama Timothy Ndanya amesema wao kama uongozi wa wilaya ya
Kahama wanafarijika na jitihada zinazofanywa na Kampuni ya Acacia
kupitia Mgodi wa Buzwagi katika harakati za kuhakikisha Jamii inajua
afya zao kwa kupima afya na kupanga maisha yao vizuri.
Ameongeza
pia jitihada hizo zimekuwa zikionekana kupitia katika sekta ya michezo
na hii imekuwa ikijidhihirisha kupitia programu mbalimbali za michezo
ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Kampuni ya Acacia.
Akizungumzia
Mashindano ya Mahusiano Cup ya mwaka huu ambayo yamehusisha timu nyingi
zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita, Katibu Tawala huyo amesema
mashindano ya mwaka huu yamesaidia kuonyesha vipaji vingi vya
wanamichezo ambao hapo awali hawakuwa na fursa ya kuweza kuonyesha uwezo
wao kupitia michezo.
“Kwetu
sisi mmeturahisishia na kwa sababu viongozi wa vyama vya michezo wako
wako hapa, hapana shaka watakuwa wamevitambua vipaji ambavyo vimekuwa
vikionyeshwa kwa muda wote wa mashindano haya na watatafuta namna nzuri
ya kuviendeleza pamoja na kutengeneza timu imara ya halmashauri ya
Kahama Mji ambayo itakuwa ikituwakilisha katika michezo mbalimbali”
Alisema Timoth.
Kwa
Upande wake kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza
amesema michezo ya mwaka huu imekuwa ya mafanikio makubwa sana na kwamba
Malengo yake yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.
“Mwaka
huu Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wa Buzwagi tulikuwa na dhamira ya
kuwafikia wakazi wengi wa Kahma kwa njia ya michezo ili kuwapatia elimu
juu ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kuimarisha Mahusiano yetu na wenyeji
wa Kahama, ndio maana utaona mwaka huu michezo hii imefanyika nje ya
eneo la kata ya Mwendakulima na kuhusisha timu za tarafa yote ya Kahama
Mji” Alisema Mkanza.
Akizungumzia
takwimu za upimaji VVU kwa kipindi cha wiki moja ambacho Mashindano
hayo ya Mahusiano Cup yalikuwa yakiendelea, Kaimu Meneja Mkuu huyo wa
Mgodi wa Buzwagi, amesema jumla ya watu 420 walijitokeza kupima VVU
ambapo kati ya hao Wanawake walikuwa 89 sawa na asilimia 21.1% na
wanaume 321 sawa na asilimia 76.4%. Ambapo kati ya wote waliopima watu
11 walikutwa na maambukizi sawa na asilimia 2.6%, Wanawake 5 sawa na
asilimia 1.19% na wanaume 6 sawa na asilimia 1.42%
Michezo
ya Mahusiano Cup ya mwaka 2016 ilifanyika katika viwanja vya
Halmashauri ya Mji wa Kahama na Uwanja wa Shule ya Msingi Mwendakulima
ambapo jumla ya timu kumi na nne za mpira wa mguu zilishiri na timu sita
za mpira wa pete.
Timu
zilizoshiriki Mpira wa Mguu:- ni kata ya Nyihogo, Nyahanga, Busoka,
Kahama Mjini, Zongomela, Malunga, Mhungula, Majengo, Mwendakulima,
Ngogwa, Nyasubi, Mhongolo, Wendele, Pamoja na timu ya Mgodi wa Buzwagi,
na kwa upande wa Mpira wa Pete:- timu za Kata za Kahama Mjini ,
Mhungula, Mwendakulima, Mhongolo, Ngogwa na Zongomela zilishiriki
mashindano hayo.
Katika
michezo hiyo zaidi ya wanamichezo 400 walijitokeza kushiriki ambapo
timu za Kahama Mji pamoja na Mhungula ndizo zilizofanikiwa kuingia
fainali, ambapo katika mchezo wa fainali timu ya Mhungula iliibuka
kidedea kwa kuibamiza timu ya Kahama mji jumla ya goli tatu kwa mbili na
kujinyakulia Kombe pamoja na Shilingi milioni moja huku mshindi wa pili
timu ya Kahama Mji kuondoka na kitita cha shilingi laki saba na nusu
pamoja na kikombe.
Kwa
upande wa timu za mpira wa pete zilizofanikiwa kuingia fainali zilikuwa
ni timu za Kahama Mji na timu za Zongomela ambapo timu ya Kahama Mji
iliibuka Mshindi baada ya kuwafunga wenzao wa kata ya Zongomela jumla ya
vikapu 47 dhidi ya 22 na Hivyo kuwafanya timu ya Kahama Mji kuwa
Washindi wa Mahusiano Cup kwa upande wa timu za netball kwa Mwaka 2016
na kujinyakulia Kombe pamoja na Shilingi milioni moja huku mshindi wa
pili timu ya Zongomela ikiondoka na kitita cha shilingi laki saba na
nusu pamoja na kikombe.
Katika
mashindano hayo hiyo timu ya Mgodi wa Buzwagi ilishika nafasi ya tatu
na kujinyakulia shilingi laki tano kwa upande wa mpira wa miguu na timu
ya Netball kutoka kata ya Mwendakuliam ilikuwa mshindi wa tatu kwa
upande wa mpira wa pete na kuondoka pia na shilingi laki tano. Huku timu
zingine zote zikiambulia kifuta jasho cha shilingi elfu sabini kila
timu.
Kabla
ya kufanyika kwa fainali hizo mapema asubuhi kampuni hiyo ya Acacia
kupitia Mgodi wa Buzwagi iliandaa pia Bonanza maalumu la Michezo
lililowahusisha wadau mbalimbali kutoka ndani ya mji wa Kahama Bonanza
lililohusisha michezo kama vile kuvuta kamba, kufukuza kuku na mpira wa
miguu.


















SHARE
No comments:
Post a Comment