Vijana
wa mikoa ya Lindi na Mtwara walioendelezwa na kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kupitia mradi wa Airtel Fursa wamesema tayari wameanza
kupata mafanikio kutokana na Ongezeko la Faida za kiuchumi ambazo
zinatokana na kuwezeshwa na kampuni hiyo.
Hali hiyo imeonekana baada ya Kampuni ya Airtel Kuwatembelea katika
maeneo wanayofanyia Biashara mara baada ya kuwawezesha na kusimamiwa na
Viongozi wa Airtel wa mkoani kwa lengo la kutazama changamoto pamoja na
mafanikio wanayoyapata.
Mkoani Mtwara mmoja wa mnufanika anaonekana kuboresha eneo lake la
biashara baada ya kufungua ofisi nyingine ili kujipatia faida maradufu
huku kikundi cha Sauti ya Jamii kilichopo Lindi kinachojishughulisha na
shughuli za kilimo na ufugaji kilipokea msaada wa mbuzi 40 kuonekana
kupata changamoyo na kuanza upya.
“Tunaishukuru sana Airtel kwa msaada wa mbuzi 40 pamoja na kutujengea
banda la kisasa hapo mwanzo, tumeeendea vyema lakini tukapatwa na
changamoto ya baadhi ya mbuzi wetu kupatwa na ugonjwa na kufa,
tulijipanga upya kwasasa tuliuza wale wote kama nyama na sasa tumenunua
mbuzi wazuri wanaweza kuzaa mapcha kila mzao, sasa tunaamini tutanza
kuona faida alisema” Salum Muunguja-Katibu kundi la Sauti ya Jamii.
kwa
upande wa mjasiliamali wa Airtel Fursa Mtwara Bi. Prisca Chilumba ambae
anafanya ujasiliamali wa Saloon saloon ya kike alisema “Mimi kwa kweli
naishukuru sana Airtel Fursa kwa kuniwezesha binafsi nimeweza kujipatia
kipato cha kunitosha na hadi sasa nimeweza kuboresha ofisi yangu na
kuhamia sehemu kubwa zaidi, pia ninamuda hata kujitangaza na kujitolea
kwa wengine kwa lengo la kupanua masoko mkoani hapa”.
Naye
meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando anasema changamoto
katika ujasiliamali ni hali ya kawaida hivyo vijana waliowengi wanapaswa
kujifunza zaidi ili kuweza kujikwamua katika dimbwi la umasikini.
Changamoto
kwa mjasiliamali ni kitu cha kawaida sana, sisi Airtel tunafanya ziara
za kuzunguka na kufahamu maendelea au changamoto za vijana wote
waliosaidiwa na Airtel FURSA ili kujua ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia
waendelee kufikia ndoto zao, tayari tumeshapita tumeshaandaa mkakati wa
kuwasaidia wote hivyo tunachotaka ni jamii pia kuwaunga mkono vijana
hawa ili waweze kufikia malengo waliojiwekea na hatimae kusaidia jamii
pia” alieleza Mmbando
SHARE
No comments:
Post a Comment