Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa
Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16
Tanzania jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya
Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na wadau
mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na
Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es
Salaam.
Meneja
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa
afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya
Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam .
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina
Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto
na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam,
katikati ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika
uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria
vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam. Picha na
Benjamin Sawe- Maelezo
SERIKALI
imezindua ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya
malaria ya mwaka 2015/16 mapema jijini Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya
tatu katika ugonjwa wa malaria ambapo ripoti imeonesha kupungua kwa vifo
vya watoto wadogo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameipongeza Ofisi ya
Taifa ya Takwimu kwa kuaanda ripoti iliyoonesha Taifa kupiga hatua
katika utoaji wa huduma ya mama na mtoto.
Waziri
Ummy ameeleza kuwa ripoti hiyo itaisaidia Wizara ya Afya na serikali kwa
ujumla katika kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa mipango endelevu
katika huduma za afya hapa nchini ili kuboresha utoaji wa huduma ambazo
ripoti imeonesha haikufanya vizuri kutokana na changamoto mbalimbali
ambazo ripoti imezibainisha.
“Ripoti
hii imeonesha kuwa bado kuna changamoto katika mimba za utotoni kwani
zimeongezeka ukilinganisha na mwaka 2010 ambapo watoto 23 kati ya mia
moja walipata mimba wakiwa na umri mdogo ukilinganisha na sasa watoto 27
kati ya mia moja hupata mimba katika umri mdogo hivyo kuna haja ya
jamii kuelimishwa juu ya madhara ya mimba za utotoni”, alisema Waziri
Ummy.
Aliongeza
kuwa kuna haja ya serikali kuangalia upya sheria ya kuruhusu mwanafunzi
kuendelea na masomo endapo akipata mimba akiwa shuleni kwani kumzuia
kuendelea na masomo ni kupoteza nguvu kazi ya taifa na kuikwamisha
serikali kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa amesema kuwa iwapo huduma za afya zitaboreshwa zitapelekea ukuaji
wa uchumi kwasababu ya uwepo wa nguvu kazi ya uhakika na kuongeza
uzalishaji kwa Taifa.
“Wananchi
wakiwa hawana afya ya kutosha na kuugua mara kwa mara uchumi wa nchi
yoyote Duniani hupungua kasi ya ukuaji kwa kuwa rasilimali fedha ambazo
zingeelekezwa kukuza sekta nyingine hupungua na hata nguvu kazi
kupungua” alisema Dkt. Chuwa.
Aidha
Dkt. Chuwa aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015
inatamka kuwa yeyote atakaepotosha Takwimu hizi kwa makusudi
atachukuliwa hatua za kisheria kupitia kifungu cha 37 cha sheria hiyo.
Utafiti
wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 1991-92 ulionyesha kuwa katika kila
watoto 1000 wanaozaliwa hai, watoto 141 walikuwa wakifariki kabla ya
kufikia umri wa miaka mitano ila utafiti huu umebaini kuwa ni watoto
67tu ndiyo wanaofariki kati ya watoto 1000.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment