Bi.Deograsia
Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu
Dodoma UDOM, hii leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa
wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa
shule ya Sekondari Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini. BMGHabari
Mtendaji
Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye, hi leo akiwasilisha
mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo
mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara.
Wanatasnia
wa filamu na maigizo mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Mtendaji
Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo (kushoto), akizungumza
wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi
wa mafunzo hayo jana. Baada ya ufunguzi alishiriki na wadau wengine
mafunzo hayo.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akizungumza
kwenye mafunzo kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara, hii leo.
Kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert
Makoye, Bi.Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na
Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini,
Bi.Joyce Fissoo
Rais wa
Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kuhoto) akiwa pamoja na
Afisa Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kulia)
wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara.
Afisa
Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kushoto)
akiwa pamoja na Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara TDFAA, Johnson
Ibambai maarufu kama Dunia (kulia), wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia
wa filamu na maigizo mkoani Mara
Wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, wakiwa kwenye mafunzo ya filamu yanayotolewa na Bodi ya Filamu mkoani humo.
Bodi ya
Filamu nchini imewataka wadau wa sekta hiyo kuwasilisha miswada ya kazi
zao ili kukaguliwa kabla ya kuanza kuigiza ili kuondona na usumbufu wa
kuzifungia kazi zisizo na maadili.
Katibu
Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fissoo, ametoa kauli hiyo kwenye mafunzo ya
siku tatu kwa wanatasnia ya filamu mkoani Mara, yanayofanyika Mjini
Musoma.
Amesema
hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu wa ambao umekuwa ukijitokeza kwa
baadhi ya miswada ya filamu kurekodiwa kabla ya kukaguliwa na baadaye
filamu zake kuzuiliwa wakati wa kuingia sokoni hivyo kuibua usumbufu
mkubwa.
Wakiwasilisha
mada kwenye mafunzo hayo, Dkt.Herbert Makoye kutoka Taasisi ya Sanaa
Bagamoyo pamoja na Deograsia Ndunguru kutoka Chuo Kikuu Dodoma,
wamewahimiza wanatasnia wa filamu kuzingatia weledi katika uandaaji wa
kazi zao kwa kuzingatia maudhui bora pamoja na maandalizi yanayokidhi
uhitaji.
Washiriki
wa mafunzo hayo wameelezea umuhimu wake ambapo wamesema yatawasaidia
kuboresha uzalishaji wa kazi zao ikiwemo kuzingatia maudhui bora tofauti
na ilivyokuwa hapo awali.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment