Wakati
Michelle Obama alikuwa mkali na mkosoaji wa Donald Trump wakati wa
kampeni, mama huyo wa Malia na Sasha amesema kuwa anaunga mkono uongozi
ujao nchini kwao. Haya aliyasema wakati anaojiwa na mtangazaji nguli,
Oprah Winfrey, siku ya jumatatu ya wiki hii kupitia kituo cha
“televisheni” CBS.
Michelle alinukiliwa akisema “Maneno tunayotamka kwa nia ya kwenda mbele, yana maana, na ndiyo sababu mimi na Barack tunaunga mkono kipindi hiki cha mpito, kwa kuwa haijalishi tunajisikiaje, ni muhimu kwa afya ya taifa kuwa tunamuunga mkono amri jeshi mkuu”
Michelle alinukiliwa akisema “Maneno tunayotamka kwa nia ya kwenda mbele, yana maana, na ndiyo sababu mimi na Barack tunaunga mkono kipindi hiki cha mpito, kwa kuwa haijalishi tunajisikiaje, ni muhimu kwa afya ya taifa kuwa tunamuunga mkono amri jeshi mkuu”
Michelle
aliongeza kwa kusema “isingefanyika wakati mume wangu (Barack Obama)
anachukua ofisi ila tunakwenda juu na hiki ndicho kilicho bora kwa ajili
ya nchi. Kwa hiyo tutasimama na rais ajae na kufanya lolote
linaliwezekana kufanyika ili kuhakikisha kuwa Trump anafanikiwa. Kwa
kuwa kama atafanikiwa, sote tunakuwa tumefanikiwa”
“First
lady” huyo wa Marekani alikutana na Melania Trump (ambae ni mke wa
Trump) katika ikulu ya White House siku chache baada ya mumewe
kuchaguliwa na kuahidi kumuunga mkono mke huyo wa rais.
"Ushauri
wangu kwa Melania ulikuwa hivi, kwa kweli huwezi kujua nini hukijui
mpaka umeingia katika majukumu haya. Kwa hiyo, mlangi uko wazi, kama
nilivyomwambia, na kama nilivyoambiwa na Laura Bush (mke wa George W.
Bush) na kama nilivyoambiwa na wake wa marais waliopita”
Michelle
alisema, timu ya Bush ilisaidia sana wafanyakazi wake muda wote wa mpito
kabla ya kuanza rasmi majukumu ya u-first lady.
Aidha
Michelle aliongeza kwa kusema "Tutafanya kila liwezekanalo ili
kuwasaidia wafanikiwe, haya ndiyo moja ya mambo niliyomwambia Melania,"
Binfasi,
nimevutiwa sana na kiwango cha uzalendo ambacho raia wa Marekani
hukionesha kwa matamko wanayoyatoa hadharani. Michelle Obama
kajipambanua kwa kusema mafanikio ya Rais wa Marekani, ni ya Wamerekani
wote na ikitokea akina Trump waki-feli basi ni Marekani yote imefeli.
Huu ni
uzalendo na kuipenda nchi ambao nasi Watanzania, kuna umuhimu wa kuiga
kwa kuwa ni jambo jema. Mafanikio ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa John Magufuli kwa namna alivyoanza mpaka sasa, ni
mafaniko yetu sote. Tuna jukumu la kusaidiana nae kwa njia yoyote ile,
ili afanikiwe. Mwalimu Nyerere alipigania uhuru, kila mmoja anafurahia
athari za nini kilifanyika zaidi ya miaka 55 iliyopita.
Tukimsaidia Rais na Tanzania ikainuka, kila mmoja anafurahia matunda ya Tanzania yenye uchumi mzuri.
SHARE
No comments:
Post a Comment