Maandamano nchini DRC ambapo takriban watu 34 wanahofiwa kufariki kulingana na shirika la Human Rights Watch
Shirika
la kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya usalama
ini DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo
yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili
kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila
ambaye alikataa kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku
ya Jumatatu.
Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini magharibi mwa Congo.
Maafisa
wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu
linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa
dunia.
Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.
Meya wa
mji huo anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo
wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga
utawala wa rais Joseph Kabila.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment