Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kodi
ili waweze kufahamu aina na madaraja ya kodi pamoja na umuhimu wa
ulipaji kodi.
Mafunzo
hayo yametolewa jana na Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA,
George Haule katika semina ya wakina mama wajasiriamali iliyoandaliwa na
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kufanyika
katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.
Haule
amesema kuwa katika uanzishaji wa biashara ya aina yoyote jambo la
kwanza na muhimu ni kujisajili katika mamlaka hiyo na kupatiwa Namba ya
Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN – Number) itakayomuwezesha mfanyabiashara
au mjasiriamali kuwa na biashara halali ambayo inalipiwa kodi kulingana
na mauzo au faida ya biashara husika.
”Tanzania
ni nchi yetu na sisi Watanzania ndio tuna jukumu la kuitunza nchi hii,
njia rahisi ya kuitunza nchi ni kulipa kodi stahiki ili kuinua pato la
taifa kwa sababu kodi ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi,”alisema
Haule.
Haule
ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inatumia mfumo endelevu wa ulipaji
kodi kwa maana ya kila mfanyabiashara mdogo mwenye mauzo yasiyozidi
20,000,000 kulipa kodi ya mwaka kulingana na mauzo yake na mwenye mauzo
yatakayozidi kiasi hicho cha fedha kulipa kodi ya mwaka kulingana na
faida anayoipata katika biashara husika.
Amefafanua
kuwa wafanyabiashara wadogo wamegawanyika katika makundi matano ambapo
wenye mauzo ya kuanzia shilingi 1 hadi 4,000,000 kwa mwaka hawalipi kodi
yoyote, wenye mauzo kuanzia 4,000,000 hadi 7,500,000 wanalipa kodi ya
shilingi 150,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia 7,500,000 hadi
11,050,000 wanalipa shilingi 318,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia
11,050,000 hadi 16,000,000 wanalipa shilingi 546,000 kwa mwaka na wenye
mauzo kuanzia 16,000,000 hadi 20,000,000 wanalipa shilingi 862,000.
Ameendelea
kufafanua kuwa mfanyabiashara mwenye mauzo ya zaidi ya 20,000,000
sheria itamtaka aandae mahesabu ya mauzo yake ili aweze kulipa kodi
kulingana na faida anayoipata kwa mwaka mmoja.
Amewaasa
wafanyabiashara kufuata sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya
ufanyaji wa biashara nchini ili kwa pamoja tushirikiane katika kuijenga
Tanzania yenye maendeleo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment