Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe
kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya
Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta
Tanzania Plc, kuanzia Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji
Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na
Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi Januari
19, 2017, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia),
akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw.
Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni
Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara
ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi,
akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara
ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa
kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia
leo Januari 19, 2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya
kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki
ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia Januari 19, 2017. Tukio
lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
Jijini Dar es salaam.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment