
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na
uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo
vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea
utendaji kazi wa vituo hivyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media
upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo
vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv jana January 17, 2017
Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake
ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo jana
January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipata
maelekezo kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa Ipp Media kuhusuana na
ufanyaji kazi wa vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo jana January 17,
2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia
studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP
Media jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa
Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba akifafanua
jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam kujionea
utendaji wake wa kazi jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na
uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Media
alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo chini ya kampuni hiyo
jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Masuala ya Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)
Frederick Ntobi akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa Sahara
Media wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye alipowatembelea jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media kwa tawi la
Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake kwa vituo vilivyo chini
ya kampuni hiyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali
imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa
habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali
yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji
kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV
na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina
ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni
muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na
Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
“Niseme
kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu
kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa
Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika
kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.
Kawa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini
ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo
vyote vya Mawasiliano Serikalini.
Dkt Abass
ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya
Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu
Serikali.
“Niwahakikishieni
ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka
Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika
vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa
kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.
Aidha
Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bibi. Joyce Mhavile ameishukuru Serikali kwa
kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari vya binafsi nchini katika
kutoa taarifa kwa umma ambazo zimesaidia kuelimisha, kuburudisha na
kutengenza mazingira ya watu kuamini yale yanayotolewa na vyombo vyao.
Naye Mkuu
wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba
ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari nchini na
kuahidi kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika upashanaji
habari.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika
ziara ya siku sita kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji
kazi wa vituo hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna
bora ya kuiendeleza sekta ya habari kwa manufaa ya taifa.(P.T
SHARE








No comments:
Post a Comment