Kaimu
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza
(ACP)Mzee Nyamka akitoa taarifa ya utendaji katika mkoa wake kwa Kaimu
Kamishna Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) mwishoni mwa juma
hili alipofanya ziara ya kiutendaji katika baadhi ya Magereza mkoani
humo.
Baadhi
ya Maafisa na askari wa Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro wakifuatilia
ufafanuzi wa hoja mbalimbali walizozitoa mbele ya Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) alipofanya ziara
kituoni hapo na kufanya Baraza la watumishi hao ili kusikiliza kero,
hoja na mapendekezo yote ikiwa ni kuboresha utendaji kazi wa siku kwa
siku.
Baadhi
ya Maafisa na askari wa Gereza Wami Kuu pamoja na Wami Vijana Mkoani
Morogoro kwa pamoja kwa makini wakifuatilia ufafanuzi wa hoja
mbalimbali walizozitoa kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma
Malewa (hayupo pichani) katika Baraza la pamoja alipowatembelea hivi
karibuni kuona utendaji kazi katika vituo vyao lakini pia kuwapa hamasa
ya utendaji kazi.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kulia)
akitembelea jengo la Karakana ya Ufundi ya Gereza Wami Vijana. Jengo
hilo pamoja na kuendelea kutumika lakini bado linahitaji kukamilishwa
kujengwa na kuwekewa miundombinu ili liweze kutoa huduma kama
ilivyokusudiwa.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akipata
maelezo mafupi ya kiutendaji kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu
Mrakibu wa Magereza (SP) Zephania Neligwa (aliyesimama) ofisini kwake
wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali Mkoani Morogoro aliyoifanya
mwishoni mwa juma.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto)
akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya Maafisa na
Askari katika kikao kilichojumuisha askari wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Morogoro na Gereza Mahabusu.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati)akisisitiza
jambo wakati wa kikao kikao chake kilichojumuisha askari wa Ofisi ya
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro na Gereza Mahabusu. Kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP)
Mzee R.Nyamka. Na kulia Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole)
Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na nawa mwisho ni Mkuu
wa Kitengo cha Uwekezaji na Ujasiliamari wa Jeshi la Magereza Mrakibu
Mwandamizi wa Magereza (SSP) Uswege Mwakahesya.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akisaini kitabu cha
wageni ofisini kwa Mkuu wa Gereza Kihonda mara alipowasili kituoni hapo
kujionea shughuli mbalimbali kituoni hapo sanjari na kuongea na maafisa
na askari wa kituo hicho mwishoni mwa Juma hili.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto)
akikagua maendeleo ya jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Gereza Kihonda.
Jengo hilo linashengwa kwa jitihada za Mkuu wa Gereza hilo kwa
kushirikiana na maafisa na askari wa kituo hicho. Viongozi wengine hapo
ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa
Magereza (ACP) Mzee Nyamka, Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation
Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na Mkuu wa Gereza
Kihonda Kamishna Msaidizi wa Magereza Ben Mwansasu.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akiendelea kusikiliza
hoja mbalimbali za maafisa na askari wa Gereza Kihonda wakati wa ziara
ya kikazi kituoni hapo. Aliyesimama ni Mkaguzi Msaidizi wa Magereza
(A/Insp) Amani Moses akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akisalimiana na baadhi ya
maafisa wa gereza Kihonda mara alipowasili akiwa tayari kufanya kikao
na watendaji wa gereza hilo.
Mmoja
wa askari wa gereza Kihonda akiwa na sura ya bashasha baada ya kupata
fursa ya kusalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza mara baada
ya kikao wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali katika baadhi ya
vituo mkoani Morogoro ikiwemo gereza Kihonda, mwishoni wa juma hili.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akikagua maendeleo ya
moja ya nyumba za zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea katika gereza la
Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za kukabiliana na
tatizo la uhaba wa nyumba kituoni hapo. Aliyefuatana naye ni Mkuu wa
Gereza la Wanawake Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Luhembe
imu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akitolea
ufafanuzi wa jambo katika kikao chake na watumishi wa gereza Kihonda
alipofanya ziara ya kiutendaji katika baadhi ya Magereza ya mkoa wa
Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro, Kamishna
Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka na kulia Mkuu wa Gereza la
Kihonda, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Ben Mwansasu.
Baadhi
ya Maafisa na askari wa Kingolwira Complex inayojumuisha Chuo cha
Uhunzi na Udereva, Gereza Mtego wa Simba, Gereza Mkono wa Mara na Gereza
la Wanawake Kingolwira katika kikao cha pamoja na Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alipofanya ziara katika vituo hivyo
kujionea shughuli mbalimbali za kila siku.
.Sehemu
ya Maafisa na askari wa vituo vya Bwawani Sekondari (inayomilikiwa na
Jeshi la Magereza) na Gereza Ubena mkoani Pwani wakiwa katika kikao cha
pamoja na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo
pichani) alipofanya ziara vituoni hapo ili kujionea shughuli za vitu
hivyo lakini pia kusiliza shida na maoni ya watumishi katika vituo hivyo
jana tarehe 28.01. 2017.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Pwani (RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP)
Boyd Mwambingu akitolea ufafanuzi moja ya hoja zilizoibuka katika kikao
cha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa na wafanyakazi
wa vituo hivyo alichofanya mwishoni mwa juma.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa gereza Wami Kuu na
Vijana alipifanya ziara ya kikazi vituoni hapo.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Mahabusu
Morogoro alipofanya ziara mkoani humo mwishoni mwa juma.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa gereza Kihonda
alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Ijumaa, 27.01.2017.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Kingolwira Complex
mara baada ya kikao kilicholenga kusikiliza kero na hoja mbalimbali za
watumishi hao, tarehe 28.01.2017.
Picha zote na ASP Deodatus Kazinja, PHQ
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa katika hali ya kuamsha
hari na morali ya kufanya kazi kwa watendaji wa Jeshi la Magereza
amefanya ziara ya kikazi katika baadhi ya Magereza ya Mkoa wa Morogoro
na Pwani mwishoni juma hili.
Ziara
hiyo imejumuisha Magereza ya Mbigiri, Wami Kuu, Wami Vijna, Mahabusu,
Kihonda, Kingolwira Complex yote ya mkoa wa Morogoro na Shule ya
Sekondari Bwawani na gereza Ubena vya mkoani Pwani.
Kutoka
kwa Kaimu Jenerali maafisa na askari aliwapata taarifa fupi ya
Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha gereza Mbigiri Mkoani
Morogoro kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF
na NSSF. Alisema uwekezaji huu ni kwa faida ya Jeshi kama Taasisi hivyo
ni vizuri kila askari akalifahamu hilo.
Katika
ziara hiyo pia alipata wasaa wa kufanya vikao na watendaji ambapo
maafsa, askari na watumishi raia walipata fursa ya kuuliza maswali moja
kwa moja kutoka kwa Mtendaji mkuu wa Jeshi la Magereza ambapo baadhi ya
mambo yalipatiwa majibu ya papo hapo na mengine kupewa ahadi ya
kutatuliwa katika siku za usoni hasa yenye uhusiano na masuala ya
kibajeti.
Miongoni
mwa masuala yaliyoonekana kuwa ni tatizo sugu ni pamoja na huduma za
maji, usafiri, matibabu kwa wafungwa na mahabusu, sare za askari, posho
mbalimbali kulingana na stahiki ya kila askari na mambo mengine madogo
madogo ambayo yote kimsingi yanagusia suala la fedha.
Katika
vikao hivyo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa
alitolea maelekezo baadhi ya mambo yaliyohitaji kauli ya Makao Makuu ya
Jeshi lakini pia aliwahakikishia kuwa ofisi yake itaendelea
kushughulikia kero zote na kusaidia kwa haraka pale inapohitaji kwa
kutegemeana na hali ya fedha kwa wakati huo.
Kaimu
Kamishna Jenerali aliwaasa maafisa askari kuwa waangalifu wanapotumia
mitandao ya kijamii hasa kwa kuzingatia viapo vya utumishi wao.“Ninyi
ni askari wenye viapo vya utii wa mamlaka zilizopo, jiepusheni na
mijadala ya mitandaoni kwani mingine iko kinyume na maadili ya kazi
zetu. Ukipokea ujumbe usiofaa futa kabisa badala ya kuusambaza”
alisisitiza Dr. Malewa
Aidha
Dr. Malewa aliwataarifu watumishi hao adhma yake kuu ya kuona Jeshi
linakuwa na hospitali kubwa nayakisasa ili kuondoa kero na aibu
inayowapata askari na familia zao wanapokuja kutibiwa Jijini Dar es
salaam.
Ni
dhamira yangu kuona tunaanzisha ujenzi wa hospitali hivi karibuni ili
kuondoka na adha ambayo wote mnaifahamu, na hospitali hii tutaijenga kwa
kutumia vyanzo mbali mbali ikiwemo na sisi kama askari kujitolea.
Naomba mtuunge mkono mara wazo hili litakapoletwa kwenu” alisisitiza
Kaimu Jenerali.
Mwisho aliwataka maafisa na askari kudumisha nidhamu kazini ikiwa ndiyo msingi mkuu wa mafanikio hasa katika kazi za majeshi.
SHARE
No comments:
Post a Comment