
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani
(Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya
Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema
leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati
za Kudumu za Bunge zimeanza shughuli zake jana ambapo katika wiki hii
takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua
miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kabla ya kurejea
Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati
Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza jambo
Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa
ziara hiyo.

Kaimu
Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo. (Picha na Ofisi ya Bunge)(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment