
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC
Wanasiasa
wa serikali na upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
wamekubaliana kuhusu sifa za Waziri Mkuu atakayeteuliwa na ukubwa wa
Baraza la Mawaziri.
Mazungumzo
hayo yamekuwa yakiongozwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki,
baada ya mkataba wa kisiasa kutiwa saini Desemba 31 mwaka 2016.
Christophe
Lutundula Apala mmoja wa wajumbe katika mazungumzo hayo ameiambia Radio
ya Umoja wa Mataifa, Radio Okapi kuwa wamekubaliana kuwa Waziri Mkuu
atakayeteuliwa, atakuwa ni mtu anayetimiza masharti ya kikatiba na
kisheria kuhudumu katika nafasi hiyo ya kisiasa.
Imekubaliwa kuwa, Waziri Mkuu atatokea katika upande wa muungano wa vyama vya upinzani vya Rassemblement.
Kuhusu ukubwa wa Baraza la Mawaziri, kutakuwepo na Mawaziri na Manaibu wao 46.
Mazungumzo
hayo yanaendelea siku ya Ijumaa, na kikubwa kinachojadiliwa ni
ugawanaji wa majukumu katika serikali mpya itakayoundwa ili kutekeleza
kikamilifu mkataba wa kisiasa.
Maaskofu nchini humo wameitaka Umoja wa Mataifasa kusaidia kufanikisha utekelezwaji wa mkataba huu.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment