
Wanajeshi wa Senegal(picha ya maktaba)
Vikosi
vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya
Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barroe anaapishwa.
Msemaji
wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye ameiambia BBC kwamba vikosi
hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi
hiyo,Banjul.Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na
ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa
vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.
Mapema
baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa
likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais
Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya
Jammeh.Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa
sasa Adama Barrow ameapishwa jana katika nchini jirani kwenye ubalozi wa
Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra
ubalozini hapo.
Mpaka
sasa haijafahamika wazi ni lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea
nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa
rais.BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment