Katibu mkuu wa shirika la umoja wa kujihami la NATO Jens Stoltenberg
anayataka mataifa wanachama kuongeza matumizi yao ya ulinzi katika
mkesha wa mkutano wa kwanza kati ya waziri mpya wa ulinzi wa Marekani
Jim Mattis na mawaziri wenzake wa mataifa 27 wanachama mjini
Brussels.Stoltenberg alisema leo kwamba ugawanaji uliosawa wa mzigo
ongezeko la matumizi katika bajeti za ulinzi ni vitu vitakavyoimarisha
umoja huo katika ya mataifa hayo yanayopakana na bahari ya Atlantic.
Rais wa Marekani Donald Trump alidokeza wakati wa kampeni ya uchaguzi
kwamba huenda asiweze kuyalinda mataifa washirika ambayo yatakataa
kuchangia kiasi kinachohitajika kutoka kwao. Matamshi yake yameyashitua
mataifa ya Ulaya , hususan yake yaliyoko karibu na mpaka na Urusi kama
mataifa ya eneo la Baltic na Poland. wakati huo huo washirika wa NATO wa
mataifa ya Ulaya na Canada wameongeza matumizi yao ya ulinzi kwa
asilimia 3.8 mwaka jana , ama dola bilioni 10 zaidi kuliko mwaka 2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment