Rais wa Iran Hassan Rouhani atafanya ziara nchini Oman na Kuwait
kesho Jumatano , ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika mataifa hayo ya
ghuba tangu kuingia madarakani mwaka 2013. Rouhani ataondoka kesho
kwenda Muscat kukutana na Sulatani wa Oman Qaboos , amesema naibu
mnadhimu mkuu wa ofisi ya rais anayehusika na mawasiliano , Parviz
Esmaeili. Atakwenda Kuwait siku hiyo hiyo kwa mwaliko wa kiongozi wa
nchi hiyo Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah. Waziri wa mambo ya kigeni wa
Kuwait aliwahi kufanya ziara mjini Tehran mwishoni mwa mwezi Januari
kuwasilisha ujumbe kwa rais Rouhani kwa misingi ya majadiliano kati ya
mataifa ya Ghuba na hasimu wao Iran. Mataifa sita wanachama wa baraza la
ushirikiano la Ghuba GCC hususan Saudi Arabia , yanaishutumu Iran kwa
kutumia madhehebu kuingilia masuala ya mataifa ya kiarabu na kujenga
ushawishi wake katika mashariki ya kati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment