Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasaliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa
(katikati) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko cha MV Kilambo kinachomilikiwa na
TEMESA Jaston Mbawala wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani
Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Mhandisi Samwel Chibwana wa TEMESA Mtwara.
Meneja
wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Mtwara Mhandisi Saidi
Mongomongo akimuelezea jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kivuko cha MV Kilambo
kilichopo mkoani Mtwara kinachotoa huduma mto Ruvuma mpakani mwa
Tanzania na Msumbiji.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua
injini ya kivuko cha MV Kilambo kinachotoa huduma mto Ruvuma kati ya
Kilambo, Tanzania na Namoto, Msumbiji. Picha na Alfred Mgweno, TEMESA
Na Alfred Mgweno, TEMESA Mtwara.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa
ametembelea na kukagua kivuko cha MV Kilambo kilichopo Mkoani Mtwara
mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Kivuko hicho kinavusha magari, abiria
na mizigo kati ya Kilambo upande wa Tanzania na Namoto Msumbiji.
Akiwa
katika ziara hiyo Profesa Mbarawa aliambatana na viongozi mbalimbali wa
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
mkoani hapa. Profesa Mbarawa alikaribishwa na Mkuu wa Kivuko hicho
Jaston Mbawala, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wa Mkoa wa
Mtwara Mhandisi Saidi Mongomongo, Mhandisi Msaidizi wa Kivuko Samwel
Chibwana pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma
za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle.
Akiwa
kivukoni hapo, Profesa Mbarawa alipata wasaa wa kusikiliza baadhi ya
changamoto zinazokikumba kivuko hicho ambapo Mhandisi Saidi Mongomongo
alitaja changamoto hizo kuwa ni upungufu wa maji nyakati za kiangazi,
ubovu wa maegesho ambayo husababisha magari makubwa kunasa wakati
yanatoka au kuingia ndani ya kivuko pamoja na kukosekana kwa boti ndogo
za uokoaji ambazo zingesaidia wakati wa dharura.
Baadae
Profesa Mbarawa alipata fursa ya kuongea na watumishi walio chini ya
Wizara yake katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa huku
akiwataka watumishi kuendelea kushirikiana na serikali, kufanya kazi
kwa kasi na uadilifu kwa kuzingatia weledi. Pia aliwataka watumishi
kujenga tabia ya kujitoa kwa ajili ya nchi yao.
Profesa
Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo kwa nia
ya kutembelea na kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya
wizara yake.
SHARE
No comments:
Post a Comment