Makamu wa rais wa Venezuela amepuuzia vikwazo vilivyowekwa na
Marekani akitajwa kuwa msafirishaji mkubwa wa madawa ya kulevywa. Katika
ujumbe uliowekwa katika mtandao wa kijamii , Tareck El-Aissami amesema
uchokozi unaochukiza na kupaka matope , unaofanywa na Marekani
hautamzuwia kufanya kazi yake ya kuimarisha mapinduzi yaliyoanzishwa na
kiongozi wao marehemu Hugo Chavez. Utawala wa rais Trump wa Marekani
jana ulizuwia mali zote zilizoko nchini Marekani za El- Aissami pamoja
na wafanyabiashara ambao imesema wanafanyakazi kama watu wake walioko
mbele katika jukumu lao la kufanikisha usafirishaji mkubwa wa madawa ya
kulenywa kutoka Venezuela. El Aissami ni kiongozi wa ngazi ya juu wa
Venezuela kuwekewa vikwazo na Marekani. Kutajwa kwake kama mbabe wa
biashara ya madawa ya kulevywa kutaongeza hali ya wasi wasi kati ya nchi
hizo mbili.
Tuesday, February 14, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment