Raisi wa Iran Hassan Rohani
Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema hii leo kuwa Iran
ni taifa kubwa linalofadhili ugaidi duniani wakati huu Rais wa Marekani
Donald Trump akiiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi karibuni
ya kufanya jaribio kombora.
Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani
ameyasema hayo katika mkutano na vyombo vya habari mjini Tokyo akidai
Marekani haina mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika eneo la
mashariki ya kati.
Aidha raisi Trump aliandika kwenye
mtandao wa twitter kuwa,Iran inacheza na moto, hawana shukran jinsi
Obama alikuwa mkarimu kwao, Si mimi!"
Lakini utawala wa Iran unasema kuwa
hauwezi kulegeza kamba kutokana na vitisho visivyo na maana vya
Marekani, kutoka kwa mtu asiye na ujuzi.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment