Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Ni jambo lisilopingika kuwa matumizi
makubwa ya fedha za Serikali yanatumika katika ujenzi wa miundombinu ya
Umma ambapo matumizi hayo yanahusisha karibu asilimia 53 ya Bajeti nzima
ya nchi.
Tunaishukuru Serikali kwa kuweka
kipaumbele katika suala hilo kwani ni muhimu kuwa na miundombinu mizuri
na bora ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kurahisisha ufanyaji kazi
hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi katika Nyanja zote muhimu zikiwemo
za biashara, utalii na mawasiliano.
Miradi ya ujenzi ya miundombinu ya Umma
inayoelezewa hapa ni ile ambayo inajengwa kwa fedha za Serikali kwa
ajili ya matumizi ya wananchi wote ikiwemo ya barabara, hospitali na
vituo vya afya,shule,vyuo,nyumba za kuishi pamoja na ofisi mbalimbali.
SHARE
No comments:
Post a Comment