Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichoko Kunduchi Dar Es Salaam, Kanali Yacub Mohamed, yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.
Kanali
Mohamed amesema atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya kuona
miundombinu yake na kubadilishana uzoefu na wakuu wa chuo hicho
kilichopo Karen katika viunga vya jiji la Nairobi.
Mkuu
huyo wa Chuo ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na kuonana na Kaimu
Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. Lengo kubwa la ziara yake ni
kubadilishana uzoefu na Chuo cha Kenya kuhusu uendeshaji na uandaaji wa
mitaala.
Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (Kulia) akifurahia
zaidi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kanali Yacub
Mohamed (wa pili kushoto). Kushoto ni Mshauri wa Kijeshi wa Ubalozi wa
Tanzania, Kanali Fabian Machemba.
Kanali
Mohamed na Kaimu Balozi (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wa
pili kulia ni Mshauri wa Kijeshi Kanali Machema na kulia ni Kanali
Maulid Surumbu kutoka Chuo cha Ulinzi. Kushoto ni Kanali Njoroge wa
Jeshi la Ulinzi la Kenya.
SHARE
No comments:
Post a Comment