Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wahanga wa Ajali ya kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa RZ uliopo katika Kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Mkoani Geita iliyotokea tarehe 26 Januari, 2017.
Aidha,
Prof. Muhongo amewataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini
kuchukua hatua za haraka kusimamia mazoezi ya uokoaji pindi zinapotokea
ajali migodini pasipo kusubiri miongozo ya Waziri.
Pia
amewaagiza Makamishna hao kufanya ukaguzi katika migodi mikubwa na
midogo katika maeneo nayo na kuongeza kuwa, zoezi hilo la ukaguzi
linatakiwa kufanywa haraka.Pia
amemtaka Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi,
kufuta leseni zote za uchimbaji madini ambazo hazifanyi kazi.
Akizungumzia
kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo chini, Prof. Muhongo amesema
kuwa, Sera na mipango ya Serikali ni kuwandeleza wachimbaji hao na
kuhakikisha kuwa, wanatoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa
Kati.
Katika
hatua nyingine, Prof. Muhongo ameitaka Migodi Mikubwa yote nchini
kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na kueleza kuwa, migodi
hiyo imepewa wiki 6 iwe imejiandikisha katika soko hilo.
Pia
Prof. Muhongo amemshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani, Mkoa wa Geita, Viongozi wa Wizara, Wachimbaji na kampuni zote
zilizoshiriki zoezi la uokoaji na kufanikiwa kuokolewa kwa wachimbaji
15 waliofukiwa na kifusi.
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya
Wahanga wa ajali ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ, Mkoani Geita.
Prof. Muhongo alifika mgodini hapo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati) akimuongoza
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake
kuelekea katika eneo la mgodi wa dhahabu wa RZ.
Mkuu
wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo
wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
Mkuu
wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo
wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
Wachimbaji
wadogo wakimwonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
na ujumbe wake namna walivyookolewa baada ya kufukiwa na kifusi katika
mgodi wa dhahabu wa RZ, uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita.
Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi akiwaongoza Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Geita
Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi
ambako wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa wote wakiwa hai.
SHARE
No comments:
Post a Comment