Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) amemaliza kufanya ziara yake ya siku tatu katika jimbo
la Shinyanga.
Katika
ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Februari 15,2017 kumalizika Februari
17,2017 ,Mheshimiwa Masele amekagua miradi ya maendeleo na kufanya vikao
na wananchi wa kata 14 kisha kujadili na kuzitafutia ufumbuzi kero za
wananchi.
Katika
maeneo mengi aliyopita,Mheshimiwa Masele amekutana na kilio kikubwa cha
tatizo la njaa linalowakabili wananchi ambao walidai wamekuwa
wakiendesha maisha yao kwa kunywa uji hivyo kuiomba serikali iwaone kwa
jicho la huruma na kuwapatia chakula.
Mheshimiwa
Masele pia amekumbana na kilio cha bei kubwa ya maji inayotozwa na
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga
(SHUWASA),huku wananchi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa
maji kutoka ziwa Victoria wakiomba huduma hiyo ili kuondokana na kero ya
maji.
Viongozi
wa shule za msingi nao walipaza sauti zao juu ya uhaba wa walimu katika
shule,matundu machache ya vyoo ukilinganisha na idadi kubwa ya
wanafunzi,upungufu wa madarasa huku wengine wakiomba kupatiwa huduma ya
maji na umeme katika shule zao.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo,Mheshimiwa Masele alisema yeye kama mbunge hayupo
tayari kunyamaza juu ya matatizo yanayowakabili wananchi wake na kuahidi
kuendelea kushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kumaliza changamoto
hizo.
“Naomba
serikali yetu itambue kuwa wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini wana
njaa,wanahitaji chakula,hatuhitaji chakula cha bure bali tunataka
chakula cha bei nafuu,wananchi wanalala njaa,shule zetu hazina walimu wa
kutosha,bado bei ya maji iko juu sana ukilinganisha na kipato cha
wananchi”,alieleza Masele.
Siku
ya kwanza ya ziara,mheshimiwa Masele alitembelea mradi mkubwa wa ujenzi
wa daraja la Galamba na kuangalia,siku ya pili na tatu katika ziara yake
ametembelea shule za msingi na kufanya vikao mbalimbali.
Mwandishi
wetu,Kadama Malunde,alikuwepo kwenye ziara hiyo…Ametuletea Picha 53 za
Matukio yaliyojiri siku ya pili na ya tatu ya Ziara ya Mheshimiwa
Stephen Masele…Tazama hapo chini
SIKU YA PILI ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI MHESHIMIWA STEPHEN MASELE
Hapa
ni katika Shule ya Msingi Twende Pamoja iliyopo katika kijiji cha
Mwamalili kata ya Mwamalili katika Manispaa ya Shinyanga.Katikati ni
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM)
akienda kuangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya wanafunzi wa
shule hiyo.Kulia ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul Machela (CCM),wa
kwanza kushoto
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiangalia eneo
ambapo patajengwa choo kwa ajili ya shule ya msingi Twendepamoja yenye
jumla ya wanafunzi 820 wanaotumia matundu 6 ya choo na walimu 8 pekee.Wa
kwanza kushoto ni mwalimu Cephrine Philip anayefundisha katika shule
hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia
wanafunzi wa shule ya msingi Twende Pamoja ambapo alisema kupitia mfuko
wa jimbo ametoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa
shule hiyo.
Hapa
ni katika shule ya Msingi Ujamaa katika kijiji cha Seseko kata ya
Mwamalili.Kulia ni Mwalimu mkuu Msaidizi katika shule hiyo Regina
Bundala akimwonesha mheshimiwa Masele eneo ambapo watajenga choo kipya
kwa ajili ya shule hiyo yenye wanafunzi 662 wakitumia matundu manne ya
choo huku walimu nane waliopo katika choo hicho wakiwa hawana choo.
Katikati
ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele
akizungumza akiwa katika ofisi ya walimu shule ya msingi Ujamaa ambapo
alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa
choo cha wanafunzi na walimu wa shule hiyo.Kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa
manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai,kushoto ni diwani wa kata ya
Mwamalili Paul Machela.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia
wanafunzi wa shule ya msingi Ujamaa na kuwataka wasome kwa bidii kwani
elimu ina faida na itawasaidia kujikomboa katika maisha yao.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa amebeba
mtoto katika ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Seseko inayotumika kama
Zahanati ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya kliniki kwa watoto
Hapa
ni katika shule ya Msingi Old Shinyanga iliyopo katika kata ya Old
Shinyanga, Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele
akikagua choo kipya (kushoto) cha wanafunzi kinachojengwa chenye matundu
8 baada ya choo cha zamani kujaa na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya
choo kipya akiangalia ujenzi unavyoendelea.Kushoto kwake ni diwani wa
tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM).
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza nje
ya choo hicho ambapo alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2.3
kusaidia katika shughuli za maendeleo ya kata ya Old Shinyanga.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika
jengo la kituo cha Maendeleo ya awali ya watoto kilichojengwa na shirika
la Save the Children kilichopo katika shule ya msingi Old Shinyanga
katika kata ya Old Shinyanga
Diwani
wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM) akielezea
changamoto zilizopo katika kata ya Old Shinyanga wakati wa kikao cha
mbunge Masele na wananchi wa eneo hilo ambapo alisema ni pamoja na uhaba
wa matundu ya vyoo, katika shule,zahanati ya Old Shinyanga kukosa
chumba kwa ajili ya akina mama wajawazito na eneo la zahanati kukosa
uzio kutenganisha na mnada uliopo katika zahanati hiyo
Mbunge
wa Shinyanga Mjini Mheshimwa Stephen Masele akizungumza wakati wa kikao
na wananchi wa kata ya Old Shinyanga kujadili na kuzipatia ufumbuzi
changamoto za wananchi.Masele alilipongeza shirika la Save the Children
kujenga jengo kwa ajili ya maendeleo ya awali ya watoto katika kata hiyo
na kwamba serikali itaendelea kusaidia katika miradi mbalimbali katika
kata hiyo.Kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini
Rajabu Makuburi
Mkazi
wa Old Shinyanga akimwelezea Mbunge Masele jinsi wakazi wa eneo hilo
wanavyoshinda na njaa kutokana na uhaba wa chakula inayochangiwa na
chakula kuuzwa kwa bei kubwa
Mheshimiwa Masele akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya msingi Old Shinyanga
Mheshimiwa
Masele akizungumza na baadhi ya vijana wa Old Shinyanga walioamua
kuzuia gari lake asiendelee na safari ili asalimiane nao
Hapa
ni katika shule ya Msingi Chibe katika kata ya Chibe manispaa ya
Shinyanga.Aliyesimama ni ni Diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa
Picca Chogelo (CCM) akizungumza katika kikao cha mbunge na wananchi wa
kata ya Chibe ambapo alisema kata hiyo haina shule ya sekondari watoto
wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwenda Old Shinyanga,eneo hilo halina
huduma ya maji huku akiomba kata hiyo ijengewe barabara kwa kiwango cha
lami kwani mji huo unakua kwa kasi
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na
wakazi wa Chibe ambapo alisema anachofanya hivi sasa ni kuhakikisha
shule zote za msingi katika jimbo lake zinamaliza changamoto ya uhaba wa
matundu cha choo
Wananchi wa Chibe wakimsikiliza mbunge wao
Wananchi wakiwa katika kikao
Hapa
ni katika kata ya Lubaga: Katikati ni diwani wa kata ya Lubaga
mheshimiwa Obeid Jilala (CHADEMA)akimpokea mheshimiwa Stephen Masele
Mheshimiwa Masele(CCM) akiwa na Obeid Jilala (CHADEMA) katika kikao cha kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero za wananchi
Diwani
wa kata Lubaga mheshimiwa Jilala akimkaribisha mheshimiwa Masele
(kushoto) ili azungumze na wananchi wa kata ya Lubaga.Kulia ni katibu
mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajabu Makuburi
Mheshimiwa
Masele akizungumza katika kikao cha majadiliano kuhusu maendeleo ya
kata ambapo alisema ametoa shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia
shughuli za maendeleo ya kata hiyo
Mheshimiwa
Masele akijibu hoja ya ongezeko la bei kubwa ya maji na kero ya maji
machafu yanayotoka kwenye mabomba ya maji ambayo yanasambazwa na
SHUWASA
Kaimu
Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai akielezea kuhusu
namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na changamoto ya uhaba wa
walimu na matundu ya vyoo katika shule mbalimbali za manispaa ya
Shinyanga
Hapa
ni katika kata ya Chamaguha:Aliyesimama ni diwani wa kata hiyo Morice
Mugini (CCM) akimkaribisha mheshimiwa Masele katika shule ya msingi
Ushirika iliyopo katika manispaa ya Shinyanga
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Ushirika Lucia Amede akielezea changamoto ya
matundu ya choo katika shule hiyo ambayo ina wanafunzi 844,matundu 6
pekee ya choo hali inayosababisha wanafunzi wapange foleni wakati wa
kujisaidia
Mheshimiwa
Masele alizungumza katika kikao na wakazi wa kata ya Chamaguha ambapo
alisema amesema pia kuna pesa kutoka mfuko wa jimbo imetolewa kusaidia
ujenzi wa choo kipya cha shule hiyo
Katibu
Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akielezea
jinsi ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoendelea kutekelezwa katika kata
mbalimbali za jimbo la Shinyanga
Mheshimiwa Masele akiangalia choo kipya inachojengwa katika shule ya msingi Ushirika
SIKU
YA TATU KATIKA ZIARA YA MBUNGE STEPHEN MASELE-Hapa ni katika kata ya
Kizumbi,pichani Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon
Kyungai akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Neema Mkanga akitoa taarifa fupi kuhusu
shule ya msingi Kizumbi kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen
Masele.Alisema shule hiyo ina wanafunzi 502,matundu ya choo 6 ya
wanafunzi,walimu 10 wanaotumia ambao hawana choo bali wanatumia tundu
moja la choo cha wanafunzi
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi
Mheshimiwa
Masele akisisitiza kuhusu huduma ya maji katika eneo hilo ambapo
alisema huduma hiyo inatakiwa iwafikie kutokana na bomba la maji kupita
eneo la kata hiyo
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi
Mzee
Paul Kashinje mkazi wa kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi akiomba
serikali iwapatie chakula kwani wanashinda na njaa kunywa uji
Mheshimiwa
akiwa katika eneo la choo cha shule ambacho kinatumiwa na walimu na
wanafunzi,eneo hilo ndipo pia patajengwa choo kipya
Mheshimiwa Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi
Mheshimiwa Masele akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Kizumbi
Hapa ni katika shule ya msingi Ibinzamata-Wanafunzi wakimpokea mheshimiwa Masele
Mheshimiwa Masele akiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa choo cha shule ya msingi Ibinzamata
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Ibinzamata Vaileth Lumelezi akisoma risala kwa
mheshimwa Masele ambapo alisema shule hiyo haina huduma ya umeme japo
nguzo za umeme zinapita hapo.Alisema shule ina jumla ya wanafunzi 965 na
matundu manne pekee ya choo
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Ibinzamata.Kulia kwake ni diwani wa kata ya Ibinzamata Reuben Kitinya
Wazazi wakimsikiliza mheshimiwa Masele
Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi wa wanafunzi
Hapa
ni katika shule ya msingi Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga,Pichani
ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Ngunila (CHADEMA) akimkaribisha
mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ili azungumze na
wakazi wa wanafunzi katika shule hiyo
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Kitangiri Chrizestom Kitale akisoma risala kwa
mheshimiwa Masele ambapo alisema shule hiyo ina wanafunzi 1265,na kwamba
inakabiliwa na uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo
Mheshimiwa
Masele akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ametoa shilingi
milioni moja kusaidia maendeleo ya kata hiyo ikiwemo ujenzi wa matundu
ya choo
Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi
Diwani wa Viti Maalum Mariam Nyangaka(CCM) akisisitiza jambo katika kikao hicho
Wazazi wakiwa kwenye kikao Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog BOFYA <<HAPA>>KUONA PICHA ZIARA YA MASELE SIKU YA KWANZA
SHARE
No comments:
Post a Comment