Rais Bashar al-Assad wa Syria ametoa kauli ya kuunga mkono hatua
iliyotangazwa hapo kabla na Rais wa Marekani Donald Trump ya kuzuia
wasafiri wa mataifa saba yenye idadi kubwa ya Waislamu ikiwemo Syria
kuingia nchini Marekani. Rais Assad amesema hatua hii haiwalengi watu wa
Syria bali ni hatua dhidi ya kile alichokiita ugaidi. Rais huyo wa
Syria amesema amri hiyo iliyotangazwa na Rais Trump itasaidia kuzuia
magaidi kuingia nchi za Magharibi ikiwa ni pamoja na Ujerumani. Rais
Assad ametoa kauli hiyo licha ya ukweli kuwa hakuna raia wa Syria
waliohusishwa na mashambulizi yoyote ya kigaidi nchini Ujerumani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment