Ukame uliosababishwa na hali ya El Nino umechangia watu wengi
kukabiliwa na njaa katika ukanda ulioko karibu na pwani mashariki mwa
Afrika. Somalia inaripotiwa kukumbwa na hali hiyo ya ukame kwa kiwango
cha juu ambapo watu kadhaa wanaripotiwa kufariki dunia kutokana na
kukabiliwa na njaa. Nchi jirani ya Ethiopia nayo pia imekuwa ikikabiliwa
na ukame kwa muda mrefu sasa huku Kenya nayo ikitangaza kukabiliwa na
hali hiyo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kiasi cha watu milioni 12
barani Afrika wanahitaji msaada wa kiutu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment