Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo leo
ametangaza ''janga la kitaifa'' kutokana na ukame mkali ambao mashirika
ya misaada yamesema umewaingiza kiasi ya watu milioni tatu katika mzozo.
Rais Farmajo ameiomba jumuiya ya kimataifa kushughulikia haraka mzozo
huo ili kuzisaidia familia na watu binafsi kutoka katika janga la ukame
na kuepusha maafa ya kibinaadamu. Shirika la Afya Duniani, WHO jana
lilionya kuwa Somalia iko katika hatari ya kukumbwa na njaa kwa mara ya
tatu ndani ya kipindi cha miaka 25. Njaa ya mwaka 2011 iliwaua kiasi ya
watu 260,000. Wakati huo huo, ukame umesababisha kuenea kwa magonjwa ya
kuambukiza kama vile kuhara, kipindupindu na surua na karibu ya watu
milioni 5.5 wako katika hatari ya kupatwa na magonjwa hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment