Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, ameiomba radhi Ujerumani kwa
kushindwa kuzuia kuchinjwa kwa mateka wa Kijerumani aliyekuwa
anashikiliwa na wanamgambo. Amesema operesheni kabambe ya ndege za
kivita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali inaendelea. Maafisa wa
Ufilipino wamesema Jurgen Gustav Kantner aliuawa kwa kuchinjwa na
wanagambo wa Abu Sayyaf kusini mwa Ufilipino baada ya muda uliowekwa kwa
ajili ya kulipa fedha ili aweze kuachiwa huru kumalizika Jumapili.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amelaani vikali mauaji hayo akisema
hicho ni kitendo cha kuchukiza. Duterte ameelezea jinsi serikali yake
inavyoshughulikia wimbi la utekaji nyara unaofanywa na wanamgambo hao
wenye itikadi kali za Kiislamu, ikiwemo ombi kwa China la kusaidia
katika doria katika eneo la bahari ya kimataifa linalopakana na kusini
mwa Ufilipino, Malaysia na Indonesia, ambako matukio ya uharamia na
utekaji nyara yamekuwa yakifanyika.
Tuesday, February 28, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment