TRA

TRA

Tuesday, February 28, 2017

Trump kuliomba bunge liongeze bajeti ya ulinzi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufanya ongezeko kubwa katika bajeti ya ulinzi. Ikulu ya Marekani imesema Trump anataka kuongeza matumizi katika jeshi la nchi hiyo kwa kiasi cha Dola bilioni 54. Trump amesema moja ya majukumu muhimu zaidi kwa serikali ya shirikisho ni bajeti ya Marekani. Afisa wa bajeti wa Ikulu ya Marekani, amesema Trump ambaye leo atalihutubia Bunge la Marekani kwa mara ya kwanza, ataliomba bunge hilo kuongeza matumizi ya Wizara ya Ulinzi katika mwaka ujao wa fedha kwa Dola bilioni 54, katika pendekezo lake la kwanza la bajeti na kupunguza kiasi kama hicho kutoka kwenye matumizi yasiyo ya ulinzi, ikiwemo kupunguza kwa kiasi kikubwa misaada kwa mataifa ya kigeni. Hata hivyo, wabunge wa chama cha Democratic na Republican ambao lazima waipitishe bajeti hiyo, wote wanalipinga pendekezo hilo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger