Afisa
Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima
mapigo ya moyo Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam
aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya
moyo. JKCI ilishiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na
kupima afya bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee
na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408
walihudumiwa katika banda hilo.
Mtaalamu
wa Afya na Mazoezi ya viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania
Waziri Ndonde akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima
magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
umuhimu wa kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya.
Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua
kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa
muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mtaalamu
wa Dawa na Tiba kutoka Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel
akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya
moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya
vyakula bora wanavyotakiwa kula ili waepukane na magonjwa
yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni
ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila
malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mratibu
wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watu wazima na magonjwa ya
saratani kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Sara
Maongezi akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima
magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
aina za saratani na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara. Hivi karibuni
Wizara hiyo ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima
afya bure kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Twaha
Dofa (aliyeshika karatasi) akitoka kupima magonjwa ya moyo katika banda
la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa
siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Pedro Pallangyo akimsikiliza mtoto Oliva Mushi aliyefika katika banda la
Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo. Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ilizindua kampeni ya
kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo Mkoani Dodoma
ambapo wananchi wa mkoa huo walipimwa afya zao bila malipo kwa muda wa
siku mbili zoezi lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri.
SHARE
No comments:
Post a Comment