Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla akifungua Mkutano wa siku tatu wa
matayarisho ya Mpango wa kupambana na maradhi ya Polio Tanzania katika
Ukumbi wa Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na Polio wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kutoka Afrika Kusini Dkt. Mercy
Kamupira akiwasilisha mada katika mkutano unaozungumzia maradhi ya Polio
unaofanyika Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
Washiriki
wa mkutano unaojadili ugonjwa wa Polio wakiwa katika picha ya pamoja na
mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla.Picha na
Makame Mshenga-Maelezo.
…………..
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Wadau
wa chanjo wa Tanzania na nchi jirani wapo Zanzibar kwa ajili ya mkutano
wa kutathmini maradhi ya polio na matayarisho ya kuandaa mpango wa
kukabiliana na maradhi hayo iwapo yatajitokeza.
Akizungumza
katika mkutano huo unaofanyika Zanzibar Beach Hotel Mbweni, Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Suleiman amesema
maradhi ya polio sio tatizao Tanzania kwa sasa, lakini bado hatupo
salama kutokana na nchi jirani kuendelea kusumbuliwa na maradhi hayo.
Amesema
Tanzania mara ya mwisho kuwa na mgonjwa wa polio ni mwaka 1997 lakini
nchi ya Somalia, Jamhuri ya Watu wa Kongo na Nigeria bado wanakabiliwa
na maradhi hayo na watu wake wanakuja kwa shughuli mbali mbali za maisha
hivyo matayarisho ya kujiandaa ni jambo muhimu.
Amewashauri
wazazi kuendelea na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya
afya mara baada ya kuzaliwa kupatiwa chanjo zote ili kuhakikisha
maradhi hayo na mengine yanayowasumbua hayarejei tena.Meneja wa Kitengo
cha chanjo Zanzibar Dkt. Yussuf Haji Makame amesema hali ya chanjo iko
vizuri baada ya asilimia 95 ya watoto wanaostahiki kupatiwa chanjo
kupatiwa chanjo hizo.
Amesema
kitengo hivi sasa kinaendelea kufuatialia kwa karibu watoto wenye umri
kuanzia miaka 15 wanapopata ulemavu wa ghafla ili kujua chanzo chake na
amewataka wazee wanapobaini kijana wao kupata tatizo hilo kumpeleka
hospitali mapema.
Mwakilishi
wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay ameipongeza Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi kubwa za kupambana na polio na kufanikiwa
kupewa cheti maalumu mwaka 2015.Amesema Shirika hilo litaendelea kuunga
mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali na ametaka juhudi za
pamoja za wadau na jumuiya za kimataifa kuhakikisha polio na maradhi
mengine yanayozuilika kwa chanjo sio tatizo tena Zanzibar.
Akifungua
mkutano huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla amewataka wadau
wa chanjo kutoridhika na hatua iliyofikiwa ya kutokomeza Polio bali
waendelee kuweka mikakati bora zaidi itakayo hakikisha maradhi hayo
hayarejei.
Mkutano
huo wa siku tatu unaowashirikisha wataalamu wa chanjo kutoka Shirika la
Afya ulimwengu (WHO) na Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) utaundaa
Kamati ya Maafa ya polio ya kujiweka tayari wakati wote kukabiliana nayo
yatakapo tokea.
SHARE
No comments:
Post a Comment