Bi.
Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na
wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi wa akaunti maalum ya JIONGEZE MARADUFU uliofanyika
katika makao makuu ya benki hiyo. Kulia ni Bi. Upendo Nkini Mkuu wa
kitengo cha masoko wa BancABC.
Bi. Joyce Malai Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na
wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akionyesha bango lililoandikwa
Jiongeze Maradufu katika uzinduzi wa akaunti hiyo maalum ya kipekee
katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es salaam.
Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC akizungumza
jambo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya
Jiongeze maradufu. Uzinduzi huo ulifanyika katika makao makuu ya BancABC
jijini Dar es salaam.
Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na
wafanyabiashara wa kati, na Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha
masoko wa BancABC wakionyesha (bidhaa) Akaunti mpya na ya kipekee JIONGEZE MARADUFU iliyozinduliwa na BancABC.
Joyce Malai akitoa ufafanuzi kuhusu akaunti maalum ya Jiongeze Maradufu iliyozinduliwa na BancABC.
JIONGEZE MARADUFU. Pata riba hadi asilimia kumi na sita
(16%)kwa mwaka katika amana hii na kujipatia fursa ya kukopa dhidi ya amana
yako.
BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua
bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba
maalum utakayojiwekea.
Katika hali ya kawaida
kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa
mabenki. Kwa kuanzia
amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida
kwani unapata riba nzuri zaidi.
Faida nyingine ni
uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia,
kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.
BancABC imechukuwa hatua
kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila
ubabaishaji.
Akiongea jijini Dar es Salaam katika
mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa
kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce
Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii
iliyopo sasa.
“Tunathamini mchango mzuri wa
wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya
kipekee kama zawadi maalum”.
Hii haina tofauti ya kupata faida ya
biashara hata kabla hujaianza! Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati
muafaka, katika muda inayohitajika haswa. Tuna hakika bidhaa hii mpya ya
kibenki itawavutia wateja wengi hasa wale walio makini”, alisema Joyce.
“Riba ya asilimia16% inayolipwa
kabla hujamaliza muda wa kuweka akiba, ni kivutio kikubwa, ambacho kitamfanya
mteja ajivue majukumu makubwa ikiwa pamoja na kulipa ada za shule, kodi ya
nyumba, usafiri au kuitumia kama mtaji kwenye biashara zingine azipendazo kwa
kuchukua mkopo ambao dhamana ni amana yako katika benki hapo kwa hapo.
“Vile vile nawasihi wale wote ambao
hawana akiba na BancABC kutumia nafasi hii na kufaidika kwa kufungua
akaunti na kupata maelezo zaidi juu ya faida ya huduma hii ya kipekee.
BancABC iko makini kukutana na wateja wake ili kujenga misingi ya mafanikio ya
pamoja“, alimalizia.
BancABC ipo tayari kutoa huduma hii kwa
wateja wake na wasio wateja kuanzia leo kwa miezi miwil.
SHARE
No comments:
Post a Comment