KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu imeiasa kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC na kampuni nyinginezo zinazotoa
huduma za mawasiliano nchini kuendelea kubuni teknolojia zenye
kurahisisha maisha ya watanzania pia kuhakikisha inasambaza huduma zake
nchini pote na kwa gharama nafuu.
Akiongea
kwa niaba ya kamati hiyo baada ya kufanya ziara ya kikazi mwishoni mwa
wiki katika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar
es Salaam,Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof
Norman Sigalla,alisema kuwa sekta ya mawasiliano inategemewa kwa kiasi
kikubwa katika kuleta mabadiliko ya maendeleo nchini.
Alisema
kuwa mbali na sekta hii kuweza kuongeza pato la taifa kwa njia ya kodi
pia inategemewa katika kuchochea huduma za maendeleo nchini kwa
kuwa mawasiliano yakiwa mazuri ni rahisi kuendelea na alitoa wito kwa
Vodacom kuendelea kubuni huduma za kurahisisha maisha kupitia mtandao
wake wa simu na kuhakikisha huduma zake zinawafikia watanzania wote
hususani wanaoishi maeneo ya vijini ambako bado
kuna changamoto ya kupata mawasiliano bora.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Alec Mulongo,aliwaelezea
wajumbe wa kamati hiyo mikakati mbalimbali ya kampuni ya hiyo ya
kuboresha
zaidi huduma zake ikiwemo kuwamilikisha watanzania asilimia 25%ikiwa ni
utekelezaji wa sheria ya EPOCA na sheria ya fedha yam waka 2016.
Mulongo
alisema kuwa Vodacom ni mtandao mkubwa unaoongoza kuwa na watumiaji
wengi nchini na huduma zake mbalimbali kupitia mtandao huu zinaendelea
kubadilisha maisha ya watanzania kwa kuwarahisishia maisha.
“Tunayo
huduma ya M-Pesa ambayo inatumiwa na watanzania wengi katika huduma za
kifedha kwa kufanya mihamala ya malipo mbalimbali ambayo imerahisisha
maisha ya watanzania na huduma nyinginezo nyingi ikiwemo intanenti
yenye kasi kubwa lengo letu likiwa ni kuwapeleka watanzania katika
ulimwengu wa kidigitali na tutaendelea kubuni huduma nyingine nyingi
kupitia mtandao wetu”.Alisema.
Mulonga
mbali na kuelezea huduma za Vodacom alisema kuwa kampuni imekuwa mstari
wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo
la ajira nchini ambapo kupitia uwekezaji wake imeweza kuajiri idadi
kubwa ya watanzania kwa kuwapatia ajira za moja kwa moja na zisizo moja
kwa moja pia kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya kujamii ya
Vodacom Tanzania Foundation imeweza kusaidia kutatua
changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani katika sekta ya
elimu na afya.
SHARE
No comments:
Post a Comment