·
Airtel yazindua bando la HATUPIMI dakika zenu za muda wa maongezi
·
Wateja wa Airtel kufurahia kuongea bila kikomo kwa siku, wiki na mwenzi
Dar es Salaam, Jumanne 21 Machi 2017, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha
wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
“Airtel
HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo
kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na
kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi
bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna
kupimiwa dakika za maongezi.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack
Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za
maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea
kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa
kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.
“HATUPIMI
Bando” itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia,
marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja
alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila
kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya
Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa
shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa
shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika
zako ongea bila kikomo
Airtel
tunaamini “HATUPIMI” ni ofa ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja
wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe
inayowapa uhuru wakuonge watakavyo bila kikomo. Aliongeza Nchunda
Kujiunga
na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI
kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “
alisisitiza Nchunda.
Airtel
imekuja na ofa yake ya HATUPIMI ikiwa ni siku chache tu baada ya
kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya Airtel Money, Vile vile airtel
wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa
huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja wake wote huduma zao popote
walipo.Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo. Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
SHARE
No comments:
Post a Comment