Katika michezo Borussia Dortmund hapo jana imeibuka na ushindi
mwembamba wa bao moja kwa bila dhidi ya Ingolstadt katika mfululizo wa
ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani almaarufu Bundesliga. Bao
lililowahakikishia ushindi Dortmund lilifungwa na mshambuliaji wake
hatari mgaboni Pierre- Emerick Aubameyang na kumfanya mshambuliaji huyo
kufikisha idadi ya mabao 23 aliyofunga msimu huu. Licha ya ushindi huo
Dortmund ambao walianza pambano hilo kwa ari kubwa walijikuta kasi yao
ikizidi kupungua huku Ingolstadt wakionekana kuimarika kadiri muda
uliposonga. Kufuatia ushindi huo wa jana Dortmund sasa wamepunguza pengo
la pointi kwa tofauti ya pointi tatu na timu inayoshika nafasi ya pili
katika ligi hiyo ya RB Leipzig.
Saturday, March 18, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment