Watu wasiojulikana waliokuwa na bunduki wamemuua msemaji wa polisi ya
Uganda Andrew Felix Kaweesi, mlinzi wake na dereva wake walipokuwa
wakitoka nyumbani kwa afisa huyo. Msemaji wa serikali Ofwono Opondo
amesema Naibu Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi Kaweesi na askari wawili
waliokuwa naye katika gari wakielekea kazini walivamiwa na watu
wasiojuliakana na kuuawa katika mtaa wa Kulambiro ulioko viungani mwa
mji mkuu Kampala.Mkaazi mmoja wa eneo hilo la Kulambiro amesema aliwaona
wanaume wanne waliokuwa kwa pikipiki mbili wakilishambulia gari la
Kaweesi kwa kulifyatulia risasi mwendo wa saa tatu asubuhi akiongeza
pikipiki hizo zilikuwa mpya na washambuliaji walionekana kuwa stadi.
Meya wa manispaa ya Kampala Charles Sserunjogi alisema alisikia milio ya
risasi kutoka nyumbani kwake ambako ni karibu na kwa
Kaweesi.Kilichosababisha mauaji hayo bado hakijajulikana. Kaweesi
alionekana mara ya mwisho hadharani siku ya Jumatano katika hafla ambapo
alikanusha ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human
Rights Watch kuwa majeshi ya Uganda yaliwaua watu kadhaa katika
shambulizi lililolenga kasri la mfalme wa Ruwenzori mwezi Novemba mwaka
jana. Wakati huohuo Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelaani mauaji hayo
na kuwekwa mara moja kamera katika miji yote mikubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment