Taiwan imepiga
marufuku uuzaji na ulaji wa paka na mbwa kufuatia visa kadhaa vya
ukatili dhidi ya wanyama na kuzua ghadhabu ya umma.
Taiwan ndilo taifa la kwanza kuweka marufu hii Barani Asia.
Sheria mpya inanuia kukabili baadhi ya imani kuhusu ulaji mbwa. Kwa mfano kuna baadhi wanaamini kumla mbwa mweusi wakati wa msimu wa baridi kunamsaidia mtu kupata joto mwilini.
Sheria hii imeungwa mkono na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, ambaye ana mbwa watatu na paka wawili.
Ulaji wa paka na mbwa umeendelea kupungua wakati jamii ikibadilisha jinsi inavyoshughulikia wanyama wanaofugwa nyumbani. Shirika linalotetea mslahi ya wanyama 'Humane Society International', limetaja mataifa ambayo yana desturi ya kula mbwa na paka.
Haya ni pamoja,Thailand, Laos, Vietnam, Cambodia na jimbo la Nagaland nchini India. Aidha desturi hii iko katika nchi za China, Korea Kusini na Ufilipino.
CHINA
Licha ya kutokuwepo na takwimu rasmi, China inaaminika kuongoza duniani katika ulaji na uuzaji wa mbwa na paka. Kila mwaka karibu mbwa na paka milioni 10 wanaaminika kuchinjwa nchini China.
Shirika linalotetea maslahi ya wanyama linasema wanyama wengi wanaibwa wakati wakionekana barabarani bila wamiliki wao.
KOREA KUSINI
Nchini Korea Kusini, nyama ya mbwa ni maarufu sana kiasi cha kitoweo chake kupewa jina la 'Gaegogi'. Inaaminika taifa hilo lina mashamba 17,000 yanayowafuga mbwa na kuuzwa kuwa chakula. Hata hivyo shinikizo za mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama zimeanza kuzaa matunda.
VIETNAM
Takriban mbwa milioni tano wanaaminika kuchinjwa na kufanywa kitoweo nchini Vietnam kila mwaka.
Ongezeko la wateja wa nyama hii limepelekea kuwepo na biashara ya magendo ya nyama ya mbwa katika nchi jirani za Thailand, Cambodia na Laos.
Shirika linalotetea haki za wanyama la 'Asia Canine Protection Alliance', limeshinikiza serikali kujaribu kumaliza biashara ya nyama ya mbwa.
Shirika hilo limesema lina ushahidi kwamba nyama ya mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu,na huenda ikasabaisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa miongoni mwa watu wanaokula nyama yake.
- Mwanamume amuuma mbwa wa mpenzi wake
- Mbwa amzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga Nigeria
- Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani
SHARE
No comments:
Post a Comment