Timu ya
soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys
imedhihirisha ubabe wake kwa wenyeji wa fainali za U-17 Afrika mwaka
huu, Gabon baada ya kuwafunga tena 2-1 katika mchezo wa kirafiki mjini
Rabat.
Mabao ya
Serengeti Boys yamefungwa na Assad Juma na Abdul Hussein na hicho
kinakuwa kipigo cha pili mfululizo vijana wa Tanzania wanawapa wavulana w
Gabon, baada ya Aprili 22 kuwafunga pia 2-1, mabao ya Kelvin Nashon
Naftali dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally dakika ya 75.
Serengeti
Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17,
zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.
Kwa
ujumla huo unakuwa mchezo wa tano wa maandalizi kwa Serengeti kujiandaa
fainali za Gabon, baada ya awali kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30
mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa
Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black
Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Serengeti
Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda
Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3
na 6, mwaka huu.
Mei 7
timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za
Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon,
Guinea, Cameroon na Ghana.
SHARE
No comments:
Post a Comment