Mkuu 
wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo akizungumza wakati 
wa zira ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na 
Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)anayesikiliza kwa 
makini na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halamshauri ya Longido,Juma 
Mhina. 
Naibu 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa 
Chama cha Walimu mkoa wa Arusha,Lootha Laizer 
Baadhi
 ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo 
Baadhi
 ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo 
Naibu 
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akizungumza jambo alipotembelea 
eneo linapojengwa soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Orendeke 
Kata ya Namanga mkoa wa Arusha,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya 
Longido,Godfrey Chongolo. 
Naibu 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kata ya 
Makuyuni wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha baada ya kukagua ujenzi wa 
Kituo cha Afya,serikali imetenga kiasi cha Sh 700 milioni kwaajili ya 
upanuzi wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu. 
Muuguzi
 katika Kituo cha Afya cha Usa River,Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga 
Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Bonifas 
Ukio(kulia)Mh.Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo 
yake. 
Naibu 
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akiagana na Mbunge wa jimbo la 
Monduli,Julius Kalanga baada ya kumaliza ziara yake mkoani Arusha. 
Mwandishi wetu,Arusha
Naibu 
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za 
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo amewataka watumishi katika halmashauri
 zote nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu 
katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Katika
 ziara yake mkoani Arusha katika halmashauri za Meru,Longido na Monduli 
alisema serikali imeshatoa fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya(Basket 
Fund)katika halmashauri hizo hivyo kukosekana kwa madawa na vifaa tiba 
sio jambo linaloweza kuvumilika.
Alisema
 miradi yote ambayo fedha zimeshaletwa na serikali kuu kwenye 
halmashauri itekelezwe mara moja ili iweze kuwahudumia wananchi.
  SHARE 
  
















No comments:
Post a Comment