Wanasema amri mpya ya Trump dhidi ya raia wa mataifa 6 ya kiislamu si tofauti sana na marufuku ya awali ambayo jaji huyo alisitisha.
Marufuku hiyo inafaa kuanza kutekelezwa alhamis ijayo, japo inakabiliwa na vikwazo chungu nzima vya kisheria kutoka kwa majimbo kadhaa yanayosema marufuku hiyo inakiuka katiba.
Lakini jaji huyo alisema kuwa ana sababu za kutofanya hivyo.
Amesema kuwa lazima walalamishi wawasilishe ombi kabla ya yeye kutoa uamuzi wake.
Idara ya haki nchini humo ilikuwa imesema kuwa kwa sababu marufuku ya kwanza ya uhamiaji ilikuwa imepingwa na mahakama jaji huyo hangeweza kutoa uamuzi wa moja kwa moja.
Wale wanaopinga maraufuku wanasema kuwa ina athari sawa na ile ya hapo awali.Wamesemakuwa hatua hiyo ni kinyume na katiba na inaharibu biashara katika jimbo la Washington.
Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Sean Spicer amesema kuwa anaamini kuwa agizo hilo jipya litaidhinishwa na mahakama.
Majimbo kadhaa pia yamewasilisha maombi ya kupinga sheria hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment