Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao
cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.
Kikao
hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip
Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao
cha Usalama na Maadili kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,Chamwino
mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani
Dodoma,pichani kati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani
Dodoma.
SHARE
No comments:
Post a Comment