TRA

TRA

Tuesday, March 28, 2017

Kathrada: Aliyepiga vita ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki akiwa na miaka 87

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

KIONGOZI  mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.

Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg "baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake".

Pamoja na Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.

Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.


                       Ahmed Kathrada aliishi miaka 26 jela



Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.

Aliachiliwa huru mwaka 1989.
Rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.

Ahmed Kathrada aliondoka bungeni 1999, lakini aliendelea kushiriki katika siasa nchini humo.

Alikosoa mwelekeo wa chama cha ANC hivi majuzi na kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger