Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amewataka
maafisa ustawi wa jamii nchini kuelekeza nguvu katika mapambano ya vita
dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, vitendo vya ubakaji, ulawiti na
mapenzi ya jinsia moja kwa kuwa vitendo hivyo vinatishia uhai na ustawi
wa jamii.
Dkt. Kigwangala ametoa wito huo jana katika maadhimisho ya siku
ya ustawi wa jamii duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya
Ustawi wa Jamii, jijini Dar es Salaam.
“Wito wangu kwenu kuelekeza
nguvu katika maeneo haya yanayotishia uhai na ustawi wa jamii. Kwa
upande wa serikali hatua madhubuti zimechukuliwa na zinaendelea
kuchukuliwa ili kutokomeza matatizo haya ambayo ni kinyume na maadili
yetu watanzania.”
“Nitumie fursa hii kuzungumzia hali ya mmomonyoko wa maadili unaolikabili taifa letu. Tunashuhudia ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya, ukatili wa kijinsia, mapenzo ya jinsia moja, mimba za utotoni na mauaji ya vikongwe na albino. Haya ni mambo yanayohitaji ufumbuzi wa kitaaluma na taaluma yenu inayowajibu na nafasi kubwa ya kukabiliana na matatizo haya,” amesema na kuongeza.
“Nazitaka halmashauri kuwapatia ofisi za faragha maafisa ustawi
wa jamii ambazo zinaendana na kazi zao. Pia mamlaka za serikali za
mitaa kuomba vibali vya ajira kwa maafisa ustawi wa jamii na wasaidizi
wao ambao wanahitajika kufanyakazi katika Kara,” amesema
Aidha, amezitaka halmashauri nchini kutenga bajeti ya kutosha ya huduma ya ustawi wa jamii kwa ajili ya kugharamia uwezeshaji wa makundi maalumu ikiwemo familia zenye dhiki, yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi na wenye ulemavu.
SHARE
No comments:
Post a Comment