Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu
wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi) alipowasili katika viwanja
vya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria katika Kikao cha siku
moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha na
Ikulu.] 24/03/2017.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama
cha Mapinduzi alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar alipohudhuria katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/03/2017.
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar
wakipitia mada mbali mbali za Kikao kabla ya kufanyika katika Ukumbi wa
Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]
24/03/2017.
Wajumbe
wa kikao cha Siku moja cha Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa
katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo kabla
ya kuanza kwa kikao hicho mwenyekiti wake akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) [Picha na Ikulu.] 24/03/2017.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha na Ikulu.]24/03/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
………………………………………………………………………
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein, leo (jana) amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya Habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya
CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bi. Waride Bakari Jabu, amesema kikao
hicho cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.
Ameeleza kwamba pamoja na mambo
mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza
kuomba ridhaa ya Chama hicho, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa
Bunge la Afrika Mashariki, kwa kipindi cha mwaka 2017 – 2022.
“ Kutokana na Chama chetu kuwa
Kinara wa Demokrasia wanachama wengi wamejitokeza kuwania nafasi hizo
ili waweze kuiwakilisha vyema CCM na serikali inazoziongoza katika Bunge
hilo muhimu
Pia Wana CCM na wananchi kwa
ujumla tukumbuke kuwa fursa hizi zisingeweza kujitokeza kama nchi yetu
ingekuwa katika mashaka na migogoro, hivyo wito wangu tuendelee kuwa
wamoja ili wenzetu waweze kutuwakilisha vyema.”, alisema Bi. Waride.
Kikao hicho kimefanyika kwa
kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo
la 2012, ambayo inatoa Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya
CCM Zanzibar, kupokea na kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa
Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.
Bi. Waride amesema jumla ya wana
CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya
Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba waruhusiwe na CCM kugombea nafasi
hizo.
Katibu huyo wa Kamati Maalum ya
NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inapaswa kuwakilishwa na
Wabunge tisa (9).
Aidha kikao hicho kilimtambulisha
Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa
CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.
Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza
majukumu yake aliyopewa na Chama ipasavyo.
Hata hivyo Kikao pia
kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana waliojitokeza kuomba
kugombea nafasi hizo muhimu za Uongozi katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama
hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment