WAZIRI wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amekutana na
mwenzake wa Uswisi hapo jana baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa kampeni
unaolenga kuwashawishi raia wa Uturuki wanaoishi nje ya nchi kushiriki
kura ya maoni itakayoamua juu ya kumuongezea mamlaka zaidi Rais wa
Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Uhusiano kati ya Uturuki na Ulaya umekuwa
katika hali ya mashaka kwa kiwango kikubwa tangu mawaziri wa Uturuki
walipozuiwa kufanya mikutano ya kampeni barani Ulaya inayolenga
kuhamamasisha waturuki wanaoishi katika nchi za Ulaya kushiriki zoezi
hilo la kura ya maoni. Waziri wa mambo ya nje wa Uswisi Didier
Burkhalter aliitaka Uturuki kuheshimu sheria za Uswisi.
Waziri huyo wa
mambo ya nje wa Uswisi alisema uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi
inayoheshimiwa na serikali ya Uswisi ambayo pia amesema ana matumaini
kuwa ni haki kwa raia wa Uturuki iwapo wataamua kushiriki zoezi la kura
hiyo ya maoni wakiwa nchini Uswisi au nchini Uturuki.
Ziara ya Cavusoglu
nchini Uswisi inakuja baada ya serikali ya nchi hiyo kukataa ombi la
mamlaka ya mji wa Zurich kufuta ziara ya waziri wa mambo ya nje wa
Uturuki katika mji huo mapema mwezi huu kwa maelezo yaliyotolewa na
vyombo vya usalama vya mji huo kuwa mkutano wa kampeni aliokuwa amepanga
kuhudhuria ungekumbwa na maandamano makubwa.
No comments:
Post a Comment