Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo
amezindua mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na
projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.
Mama
Samia amesisitiza kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo na matumizi sahihi ya
vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuinua kiwango cha
Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini
Aidha
Makamu wa Rais amepongeza jitihada na ubunifu wa Mbunge wa Jimbo hilo la
Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Ndg
Anthony Mavunde na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika
kuwahudumia wanadodoma Mjini.
Pamoja
na hilo Mama Samia ameahidi kuunganisha Jimbo la Dodoma Mjini na mpango
wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia watoto wa kike kupitia mfumo wa
ufundishaji kidigitali wa Sillicon Valley.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Pro Futuro Bi.
Rosemary Terry (kushoto) juu ya Vishikwambi (Ipad) vitakavyotumika
katika kufundishia shule 10 zilizopo ndani ya jimbo la Dodoma mjini,
kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Anthony Mavunde . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kutoka kushoto) pamoja na
wageni waalikwa wengie wa meza kuu wakionesha baadhi ya Vishwambi mara
baada ya kuuzindua mpango huo wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets"
5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma
Mjini.
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wageni waalikwa
mbalimbali kwenye hafla fupi uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa
Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za
Jimbo la Dodoma Mjini.
Baadhi ya Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini tukio hilo
Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo adhimu kwao
SHARE
No comments:
Post a Comment