Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti)
akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt.
Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na
Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la
Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba
yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi
zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo
vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa
Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa
zao. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa
Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano
uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo,
Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa
mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi
zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo
vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa
maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa
zao.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa
hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua
Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia
ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu,
ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es
Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais
John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa
nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali
yake za ununuzi wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo
linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith
Mallya.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa
Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika
Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es
Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni
aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika
kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato
zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika
uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia
waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt.
Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo,
Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa
Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa
Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo
vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi
hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment