Umoja wa Ulaya unajiandaa kujibu taarifa ya Uingereza ya mpango wake
wa kutaka kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo baada ya nchi hiyo
kuwasilisha taarifa hiyo hapo jana mjini Brussels, Ubelgiji. Rais wa
baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema umoja huo unaozijumisha
nchi 28 utatoa jibu katika saa 48 zijazo. Wakati huo huo Rais wa
halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker amesema amesikitishwa
na uamuzi wa Uingereza wa kutaka kujiondoa Umoja wa Ulaya lakini
ameelezea matumaini yake kuwa Uingereza itajiunga tena na Umoja huo.
Bwana Juncker aliwaambia waandishi wa habari kwamba siku itakuja ambapo
Uingereza itarejea kwenye Umoja wa Ulaya. Ujerumani na Ufaransa nchi
zenye nguvu katika Umoja huo zimesisitiza juu ya kujijenga haraka kwa
nchi zitakazobakia kwenye Umoja wa Ulaya baada ya Uingereza kujitoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment