Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga,
Martin Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi
kwa kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya
Ukimwi.
Amesema Utafiti huo utaangazia pia
kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya
Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.
Amesema Tafiti tatu zilizotangulia
zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti
na utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa kipekee ambapo kwa mara ya
kwanza wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa watahusihwa.
Kwa upande wake, Meneja Takwimu
Mkoa wa Tanga, Tonny Mwanjoto, aliwataka Makatibu Tawala kuhakikisha
wanatoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi shuleni kutokomeza
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Alisema kufanya hivyo itasaidia
juhudi za Serikali kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ikiwa na
pamoja na kuyatokomeza moja kwa moja.
Wajumbe wa mkutano wa Wadau wa
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi 2016 /2017 wakifuatilia mada
zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Makatibu Tawala kutoka Wilaya za Tanga na
Wawakilishi wa TACAIDS pamoja na Wadau wa Maendeleo uliofanyika leo
ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.
Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga,
Tonny Mwanjoto akizungumza na waandishi wa habari wa Tanga mara baada ya
kuisha kwa mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashria na Matokeo ya Ukimwi
2016/ 2017.
blog ya kijamii ya tangakumekuchablog, 0655 902929
SHARE
No comments:
Post a Comment