STAA
wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka kuwa hana mpango
na hategemei mapedeshee kuendesha maisha yake kwani madhara yake ni
makubwa.
Thea
alisema katika maisha yake hajawahi kutegemea wanaume mapedeshee
wamwendeshee maisha yake kwani kuna hasara kubwa kwa sababu mastaa wengi
wa kike wanaoishi kwa kuwategemea hujikuta wakiachwa na kurudi chini
kabisa hivyo ni funzo kubwa.
“Siwezi
na sijawahi kutegemea mapedeshee kuendesha maisha, mastaa wa kike wengi
tumewaona wakiendesha magari ya thamani, wakiishi kwenye nyumba nzuri
lakini wanapoachwa wananyang’anywa kila kitu, wanafilisika wanarudi
chini, mimi tangu nimetengana na Mike Sangu sijawahi kumwanika mwanaume
yeyote kwamba ni mpenzi wangu,” alisema Thea.
SHARE
No comments:
Post a Comment