Muonekano wa Picha ya Mtambo wa kisasa wa ED –XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ambao umezinduliwa rasmi Mkoani Mbeya. |
Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog
OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali, leo imezindua na kusimika mtambo mpya wa ED-XRF utakao
tumika kufanya uchunguzi wa sampuli na vielelezo mbalimbali vikiwemo vya makosa
ya jinai.
Akizungumzia Mtambo huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa
Samweli Manyele,alisema lengo kuu ni kurahisisha shughuli za kimaabara pamoja
na usimamizi wa sheria zilizo chini ya wakala hiyo.
Alisema, baadhi ya kazi zitakazofanywa na maabara hiyo ni
kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa, sampuli za mazingira, sampuli
zinazohusisha makosa ya jinai kama vile sampuli za vinasaba na dawa za kulevya.
“Awali vipimo vya namna hii vilikuwa vikifanyika Jijini
Dar es Salaam tu, ofisi za mikoa zilikuwa zikifanya kazi ya kukusanya sampuli
na kusafirisha lakini sasa mtambo huu, umesimikwa Mbeya na utatumiwa na Mikoa
ya Nyanda za Juu Kusini kufanya kazi hiyo“alisema
Amesema maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ni taasisi
pekee ambayo inafanya uchunguzi wa vielelezo vya sayansi ya makosa ya iinai ili
kusaidia vyombo vya sheria hususani jeshi la polisi na mahakama katika kufanya
uchunguzi ili kutoa haki kwa jamii.
“Maabara inachaangia katika kutekeleza sera ya afya ya mwaka
2007 kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara
kwa kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa zinazo zalishwa viwandani “alisema
Profesa Manyele.
Amesema maabara ya Mkemia mkuu wa serikali inasimamia
utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa udhibiti wa kemikali na majumbani
sura 182 na sheria ya usimamizi wa
teknolojia ya vinasaba vya binadamu sura 732009.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul
Ntinika ametoa wito kwa viwanda ,mashirika wajasiriamali na wananchi kwa ujumla
kutumia huduma zinazotolewa na maabara ya mkemia mkuu wa serikali ili kuhakiki
ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul Ntinika akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED –XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara leo Machi 10 katika hospital ya Mkoa jijini Mbeya. |
SHARE
No comments:
Post a Comment